Kuelekea mchezo wa marejeano wa African Football League kati ya Al Ahly dhidi ya Simba SC jijini Cairo, kuna taarifa inayotembea kwenye mitandao ya kijamii ikisema, CAF imethibitisha kuwa hakutakuwa na faida ya magoli ya ugenini katika michuano hii.
Hivyo mtu mwenye nafasi ya kutinga hatua ya nusu fainali kati yao ni yule atakayeshinda mchezo wa marejeano na si vinginevyo.
NB: Katika Habari hii kilichosemwa na CAF katika kiungo hiki kutoka website yao rasmi https://www.cafonline.com/news/late-drama-as-simba-and-al-ahly-draw-in-opening-afl-thriller
Inakinzana na kilichosemwa na AFL katika website yao Rasmi pia kwenye kiungo hiki https://afl.africa/simba-ahly-plot-on-all-out-approach-in-cairo-return-leg
Wakati taarifa ya kwenye website ya AFL imepostiwa siku moja baada ya taarifa ya CAF kupostiwa
Inawezekana ikawa ni tetesi kwa watanzania na wanasimba kwa ujumla kutokana na hali ya mchezo ilivyo ila taarifa kamili ikitoka tutakuthibitishia hapa hapa sokaleo.com
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE