Nyota watatu wa Yanga wamerejea kikosini kwa ajili ya kuanza maandalizi ya kuivaa Azam FC, ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu unaotarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam, Oktoba 25.
Metacha Mnata, Farid Mussa na Jonas Mkude hawakuhusika kwenye mechi tatu zilizopita kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo matatizo ya kifamilia na utovu wa nidhamu, lakini sasa wameitwa kambini kujiandaa na mechi zijazo.
Metacha na Mkude walidaiwa kusimamishwa kutokana na utovu wa nidhamu, huku Farid akiwa na ruhusa maalumu na kukosa mechi ya marudiano dhidi ya Al Merreikh, Ihefu na Geita Gold.
Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi aliliambia gazeti hili jana kuwa atatumia kipindi hiki cha mapumziko kuboresha kikosi chake na kuleta usawa.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE