Home KITAIFA MUHIMU KUWA NA MAANDALIZI BORA KILA WAKATI

MUHIMU KUWA NA MAANDALIZI BORA KILA WAKATI

0
maandalizi

MWENDELEZO mzuri unahitajika kwa wachezaji wote katika mechi ambazo wanacheza. Hali bado haijawa nzuri kwa baadhi ya wachezaji kufikiria mpira ni matumizi ya nguvu kubwa mwanzo mwisho.

Ipo wazi kuwa mpira wa mchezo huwezi kuacha kutumia nguvu lakini ni muhimu kuwa makini. Kwenye msako wa pointi tatu ila ni muhimu kuwa makini katika kutimiza majukumu.

Wapo wachezaji wanaopata maumivu wakiwa kwenye kutimiza majukumu yao. Kukaa kwao nje ya uwanja kwa ajili ya kupambania hali zao kunawarudisha nyuma katika kupambania malengo yao.

Muda ni sasa kufanyia maboresho ya kile ambacho mnafundishwa uwanjani. Hakuna mwalimu ambaye anafundisha kuwachezea faulo wengine uwanjani hivyo huwa ni hulka kwa wachezaji.

Inachotakiwa kila mchezaji kuongeza nidhamu kwenye mechi ambazo anacheza na inawezekana ikiwa kila mmoja atakuwa makini kusaka ushindi.

Mechi zina ushindani mkubwa na kila mchezaji anapenda kuona timu inapata ushindi. Kupata matokeo ni maandalizi mazuri na kinachotakiwa ni kutumia makosa ya wapinzani.

Mashabiki wanapenda kuona kila ambacho kinapatikana uwanjani kinawapa furaha hata wachezaji wao wanaowapenda wanafurahi kuwaona wakitimiza majukumu yao.

Kushindwa kuendelea kuwa uwanjani kwa muda ni jambo ambalo linawaumiza sio benchi la ufundi pekee bali mpaka mashabiki nao wanapata tabu.

Ni muda kuwa makini katika kutimiza majukumu huku wachezaji wakilindwa kwa umakini. Muda ni sasa kila mchezaji kupunguza matumizi ya nguvu zisizo za lazima.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here