Home KIMATAIFA MWAMBA HUYU HAPA KUTOKA CHIPOLOPOLO AIUNGA MKONO POWER DYNAMO DHIDI YA SIMBA

MWAMBA HUYU HAPA KUTOKA CHIPOLOPOLO AIUNGA MKONO POWER DYNAMO DHIDI YA SIMBA

0

Gwiji wa Timu ya Taifa ya Zambia ‘Chipolopolo’ na TP Mazembe, kiungo fundi Rainford Kalaba ameiunga mkono Power Dynamos kuifunga Simba SC ya Tanzania wikendi hii katika mchezo wa mkondo wa pili wa Ligi ya Mabingwa Afrika wikendi hii.

Ikumbukwe Kuwa Dynamos ina mlima mkubwa wa kupanda baada ya kutoka sare ya 2-2 nyumbani katika mechi ya kwanza. Walifunga Goli La Kwanza kupitia kwa Joshua Mutale na Cephas Mulombwa, lakini juhudi zao zikazimwa na Clatous Chama, aliyefunga mabao yote Mawili Ya kusawazisha

Huku kukiwa na uchezaji mkali unaohitajika ili kusonga mbele kwa raundi zinazofuata, Kalaba anaiambia Duniayetu kwamba bado haijakamilika kwa Aba Yellow.

“Wasahau Kuhusu Matokeo Ya Kwanza, Wachukulie Kama Zile ni Dakika 45 Za Kipindi Cha Kwanza, Na Ni rahisi Power Dynamos Kuwafunga Simba sc Pale Tanzania Kuliko Simba Sc Kuwafunga Yeah Maana Wao Watakuwa Na Presha Kubwa Mbele Ya Mashabiki Wao” Alisema Rainford Kalaba

Aliongeza na Kusema; “Katika Mpira Lolote Linawezekana, Na Hakuna Timu Isiyofungika na Kama Mliwafunga goli 2 Mchezo Wa Kwanza Basi Mnaweza Kuwafunga Zaidi Ya Goli 2 maana Tayari Mnawajua Wapi Wako bora na wapi Wanaudhaifu.”

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here