Home HABARI ZA YANGA LEO MWAMNYETO: NDOTO ZIMETIMIA LIGI YA CAF

MWAMNYETO: NDOTO ZIMETIMIA LIGI YA CAF

0
Mwamnyeto

Mchezaji kutoka klabu ya Yanga na Kaptain wa kikosi hicho Bakari Nondo Mwamnyeto kwa mara ya kwanza amefunguka baada ya mchezo waliocheza juzi katika uwanja wa Azam Complex dhidi ya Al Merrikh.

Mwamnyeto amesema “Nimefurahi sana kila mchezaji katika mchezo nilikuwa na hamu ya kuona timu inasonga mbele na kwa jitihada na uwezo wa Mungu tumefanikiwa,”.

“Huko tunakoenda ndio kugumu zaidi, ila tutapambana tutafika mbali na kuiwakilisha nchi vizuri maana ni jukumu letu kama wachezaji kupambana kupata matokeo, hatua ya makundi sio mchezo maana timu zote zinakuwa bora.”

“Tulivyoteleza mwaka jana viongozi waliona upungufu uko wapi na sisi wachezaji tulipambana tukashindwa kufikia hatua hii Ligi ya Mabingwa msimu huu tukakubaliana tupambane kweli kweli na Mungu kasikia dua zetu,”

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here