Kiungo Mzamiru Yassin ni kama ndiye aliyemuingiza mwenzake Sadio Kanoute uwanjani ambapo mara baada ya Simba kupata bao aliwafuata makocha wake na kuwashauri aingie Kanoute.
Hata hivyo, Kocha Robertinho alimtaka kusubiri, lakini mara baada ya bao hilo Dynamos walishambulia na Mzamiru aliinuka tena na kuwataka makocha wamuingize Kanoute huku kocha akimfokea.
Mara baada ya muda ushauri huo ulikubalika na Mzamiru aliposikia Kanoute anaitwa aliinuka haraka na kumtaka kuharakisha kuvaa ili aingie.Kuingia kwa Kanoute kulizima nguvu ya Dyanamos ambao walikuwa wanatengeneza mashambulizi makali kwenda kwa wenyeji wao.