Home HABARI ZA SIMBA LEO SAMIA KUWAPA SIMBA SH MIL 10 KILA BAO

SAMIA KUWAPA SIMBA SH MIL 10 KILA BAO

0
Goli la Mama

Rais Samia Suluhu Hassan ameahidi kutoa zawadi ya Sh 10 milioni kwa kila goli litakalofungwa katika mchezo wa African Football League kati ya Simba SC dhidi ya Al Ahly.

Mchezo huo wa ufunguzi utapigwa 12:00 jioni dimba la Mkapa, Jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa ametoa taarifa hiyo alipozungumza na waandishi wa habari akiwa kata ya Mbagala, Wilaya ya Temeke Mkoa wa Dar es Salaam, ambako Simba wanaendelea na hamasa kuelekea mchezo huo.

“Kwenye michuano hii ya AFL, mheshimiwa Rais ameahidi, Simba katika kila goli moja, atatoa Sh milioni 10.” Amesema Msigwa.

Hatua hiyo ni muendelezo wa Rais Samia kuweka jitihada na hamasa kwenye michezo, kama ilivyokuwa msimu uliopita ambapo alikuwa akitoa Sh milioni 5-10 kwa kila bao lililofungwa na Simba SC na Yanga kwenye michuano ya CAF ngazi ya klabu.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here