Home KITAIFA TP MAZEMBE YATOLEWA AFL, ESPERANCE KUCHEZA NA WYDAD NUSU FAINALI

TP MAZEMBE YATOLEWA AFL, ESPERANCE KUCHEZA NA WYDAD NUSU FAINALI

0
TP Mazembe

TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imesukumizwa nje ya michuano ya African Football League kufuatia kipigo cha jumla cha 3-1 dhidi ya vigogo wa Tunisia, Esperance de Tunis.

FT: ESPERANCE 3-0 TP MAZEMBE (Agg. 3-1)
45’—⚽️ Oussema Bouguerra
76’—⚽️ Oussema Bouguerra
86’—⚽️ Mohamed Tougai

Mazembe ilishinda 1-0 katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa katika dimba la Benjamin Mkapa kabla ya kukubali kichapo cha 3-0 ugenini katika dimba la Olympique Hammadi Agrebi mjini Rades, Tunisia.

Esperance imetangulia nusu fainali kucheza na Wydad Casablanca.

Wydad Casablanca imetinga hatua ya nusu fainali ya African Football League kufuatia ushindi wa jumla wa 4-0 dhidi ya Miamba ya Nigeria, Enyimba FC katika dimba la Mohamed wa 5, Casablanca.

FT: WYDAD AC 3-0 ENYIMBA (Agg. 4-0)
⚽ Ayoub El Amloud 4′
⚽️ Jamal Harkass 38′
⚽️ Attiyat Allah 43′

Wydad ilishinda 1-0 katika mchezo wa mkondo wa kwanza huko Nigeria kabla ya kushusha kipondo cha 3-0 nyumbani na kuifuata Esperance ya Tunisia kwenye nusu fainali.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here