Home HABARI ZA AZAM FC LEO UBORA WA AZAM WAJULIKANA, DODOMA JIJI WAUDHIBITI VYEMA

UBORA WA AZAM WAJULIKANA, DODOMA JIJI WAUDHIBITI VYEMA

0
Dodoma jiji na Azam fc

KOCHA msaidizi wa Dodoma Jiji, Kassim Lyogope amesema kuwa ubora wa Azam FC upo kwenye viungo na hapo walipambana kuwabana wasipige pasi ndefu Kwa washambuliaji.

Ni Idris Mbombo alikuwa miongoni mwa washambuliaji waliopata nafasi ya kuonyesha makeke yake Uwanja wa Jamhuri,Dodoma.

Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Dodoma Jiji 0-0 Azam FC hivyo wakagawana pointi mojamoja.

Ni mchezo wa kwanza kwa Azam FC kukomba pointi moja ugenini ikiwa ni mara ya kwanza kwa msimu wa 2023/24 kutoka Azam Complex.

Kwenye mechi tatu ambazo Azam FC ilicheza ikiwa Uwanja wa Azam Complex ilipata ushindi mechi zote na kukomba pointi tisa mazima.

Kocha huyo amesema:”Azam FC ni timu bora na tulitambua hilo hivyo tuliwabana viungo wao wasipate nafasi ya kucheza eneo la kati na kupiga pasi ndefu.

“Hapo mpango wa kwanza ulifanikiwa na walikuwa wakibadili mbinu ka kucheza kupitia pembeni na mwisho tukapata pointi moja,”.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here