CR Belouizdad ambao ni wapinzani wa Yanga katika mechi ya kwanza ya makundi ya CAFCL wamemtimua kocha wao mkuu Sven Vandenbroeck mapema hii leo ikiwa ni tahadhari kuelekea mechi hiyo itakayopigwa wiki mbili zijazo.
Taarifa ya klabu hiyo ya Algeria iliyotolewa nusu saa iliyopita imeeleza kuwa sababu ya kuachana na kocha huyo ni kutofautiana mtazamo kati ya kocha huyo na viongozi wa klabu hiyo ambayo ni mabingwa watetezi wa Algeria.