• About Us
  • Blog No.1 Kwa Habari za Michezo na Burudani
  • Contact Us
  • Privacy Policy
Saturday, December 9, 2023
SOKALEO
  • HOME
  • KITAIFA
  • KIMATAIFA
  • MAGAZETI LEO
  • TETESI ZA USAJILI
No Result
View All Result
SOKALEO
  • HOME
  • KITAIFA
  • KIMATAIFA
  • MAGAZETI LEO
  • TETESI ZA USAJILI
No Result
View All Result
SOKALEO
No Result
View All Result

YANGA, AZAM NI MECHI YA KISASI NA KILELENI

Chikao by Chikao
October 23, 2023
in HABARI ZA AZAM FC LEO, HABARI ZA YANGA LEO, KITAIFA
0 0
yanga vs azam
Share on FacebookShare on WhatsappShare on Telegram

Ligi Kuu Bara inaendelea leo kwa mchezo mmoja kupigwa ambapo macho na masikio ya mashabiki wa soka nchini yataelekezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa wakati Yanga itakapokuwa inaikaribisha matajiri wa jiji la Dar es Salaam, Azam FC.

Mchezo huu utakaopigwa saa 12:30 usiku unatazamiwa kuleta upekee kwani timu yoyote itakayoshinda itaongoza ligi ambapo Yanga itafikisha pointi 15 sambamba na Simba ingawa zitatofautiana zaidi kwenye michezo na mabao ya kufunga na kufungwa.

Kwa upande wa Azam ambayo haijapoteza mchezo wowote kati ya mitano iliyocheza, endapo itashinda pia itafikisha pointi 16 na kukwea kileleni jambo ambalo linaongeza msisimko na ushindani mkali kwa miamba hii wakati itakapokuwa inapambana leo.

Mechi hii ni kisasi zaidi kwa Azam kwani mara ya mwisho ilipokutana na Yanga ilikuwa ni Agosti 9, mwaka huu katika Kombe la Ngao ya Jamii hatua ya nusu fainali na kupoteza mabao 2-0, mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga.

Kama haitoshi katika Ligi Kuu Bara mara ya mwisho zilipokutana Azam ilipoteza pia mabao 3-2, mechi iliyochezwa Desemba 25 mwaka jana kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa mabao yaliyofungwa na Fiston Mayele, Stephane Aziz KI na Farid Mussa.

Mabao mawili ya Azam katika mchezo huo yalifungwa yote na kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Abdul Suleiman ‘Sopu’ dakika ya 27 na 47.

ShareSendShare
Previous Post

HIZI HAPA SILAHA ZA GAMONDI DHIDI YA AZAM FC

Next Post

MCHEZO WA MAREJEANO AL AHLY NA SIMBA, HAKUNA GOLI LA UGENINI, UKWELI WA MAMBO HUU HAPA

Related Posts

ihefu
KITAIFA

MASHUJAA MAMBO SIO MAMBO, HUKU IHEFU NAO WAFUFUKA KIMASIHARA

December 8, 2023
Ahmed Ally
KITAIFA

AHMED ALLY: NGOMA IKIWA NGUMU TUPATE ALAMA MOJA TU

December 8, 2023
lomalisa
KITAIFA

MAJEMBE YATAKAYOCHUKUA NAFASI YA MWAMBA LOMALISA

December 8, 2023
Simba chama
KITAIFA

MTEGO WA CHAMA DHIDI YA WYDAD UMEKAA HIVI

December 7, 2023
Load More

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Search Here

No Result
View All Result
ihefu

MASHUJAA MAMBO SIO MAMBO, HUKU IHEFU NAO WAFUFUKA KIMASIHARA

December 8, 2023
Ahmed Ally

AHMED ALLY: NGOMA IKIWA NGUMU TUPATE ALAMA MOJA TU

December 8, 2023
Pogba

POGBA KUKABILIANA NA KIFUNGO CHA MIAKA 4

December 8, 2023
lomalisa

MAJEMBE YATAKAYOCHUKUA NAFASI YA MWAMBA LOMALISA

December 8, 2023
Anza siku yako kimichezo kwakupitia ukurasa wa mbele wa gazeti la Mwanaspoti leo tarehe 8 December 2023, Pitia vichwa vya habari na ujipatie nakala yako leo.

TUNAANZIA HAPA!, GAMONDI MZUKA,MATAJIRI WASHTUA – MWANASPOTI LEO

December 8, 2023
Simba chama

MTEGO WA CHAMA DHIDI YA WYDAD UMEKAA HIVI

December 7, 2023

Msimamo wa Ligi Kuu

SOKALEO

© 2023 SOKALEO TANZANIA | All Rights Are Reserved

  • Home
  • Privacy Policy
  • Contact Us
  • About Us

No Result
View All Result
  • HOME
  • KITAIFA
  • KIMATAIFA
  • MAGAZETI LEO
  • TETESI ZA USAJILI

© 2023 SOKALEO TANZANIA | All Rights Are Reserved

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In