Home HABARI ZA AZAM FC LEO YANGA NA AZAM ZAINGIA MTEGO WA KUKAA KILELENI MWA LIGI

YANGA NA AZAM ZAINGIA MTEGO WA KUKAA KILELENI MWA LIGI

0

Derby ya kibabe inatarajiwa kuunguruma Jumapili katika Uwanja wa Azam Complex Chamazi Jijini Dar es Salaam ikiwa na vita ya kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu.

Mtanange huo wa kukata na shoka Yanga ndiye mwenyeji ambaye anatumia uwanja wa nyumbani wa mpinzani wake, Azam. Mashabiki wa soka masikio yao ni katika dakika 90 za mchezo huo kutokana na rekodi iliyonayo Yanga kwa Azam FC.

Vita hiyo endapo Yanga ikishinda mchezo huo itaongoza ligi kwa pointi 15, ikiwazidi watani zao Simba wenye pointi kama hizo, lakini ikiwa na mabao mengi (15) ikiruhusu mawili pekee wakati Simba ikifunga mabao 14 na kuruhusu manne.

Azam inatakiwa kushinda mchezo huo ikizingatia iko nyumbani na endapo itavuna pointi tatu itaishusha Simba kileleni kwa kufikisha pointi 16. Endapo Yanga itatoka sare itakuwa na pointi 13 ambazo hazitaivusha huku Azam itakuwa na pointi 14 zitakazoifanya ishindwe kukaa kileleni mbele ya Simba.

Ili kuiondoa Simba katika nafasi hiyo wababe hao wanatakiwa kushinda mchezo huo na endapo itakwama, basi vita hiyo itakosa mshindi. Mbali na vita ya kukaa kileleni mwa msimamo lakini pia mchezo huo utawakutanisha ndugu wa zamani, Yannick Bangala ambaye hakubahatika kucheza mchezo uliopita wa Ngao ya Jamii ulioikutanisha miamba hiyo jijini Tanga huku Feisal Salum ‘Fei Toto’ akisubiriwa kwa hamu.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here