Home HABARI ZA YANGA LEO YANGA YAVUNJA REKODI YAKE KIMATAIFA

YANGA YAVUNJA REKODI YAKE KIMATAIFA

0

YANGA imetinga hatua ya makundi katika Ligi ya Mabingwa Afrika kwa ushindi wa bao 1-0 Al Merreikh.

Ni bao la Clement Mzize ambaye ni mzawa alipachika bao hilo dakika ya 66.

Jumla Yanga imefunga mabao 3-0 baada ya ule wa ugenini kupata ushindi wa mabao 2-0.

Miguel Gamondi Kocha Mkuu wa Yanga amevunja rekodi ya timu hiyo kukwama kutinga hatua ha makundi kwa Muda wa miaka 25.

Rekodi mpya imeandikwa 2023, ikivunjwa rekodi mbovu iliyokuwa kwa timu hiyo katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ofisa Habari wa Yanga Ali Kamwe aliweka wazi kuwa ukubwa wa Yanga na uwezo wa wachezaji ni muhimu kuandika rekodi mpya.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here