Home KIMATAIFA FAMILIA ZA KIAFRIKA ZINATUTIA UMASIKINI

FAMILIA ZA KIAFRIKA ZINATUTIA UMASIKINI

0
John Obi Mikel

Mchezaji wa zamani wa Chelsea na Nigeria, John Obi Mikel amelalamimka kwamba pindi ukifanikiwa ukiwa Ulaya basi utakumbana na presha kubwa kutoka kwa Familia zetu za Kiafrika maana watakuomba fedha kila muda na usipofanya hivyo basi utaonekana una roho mbaya hali inayopelekea wengi kuishia kuwa masikini tu

“Hatuzungumzi sana kuhusu hili lakini linawaharibu Wachezaji Kisaikolojia, ukipata fedha zinakuwa sio zako ni za ndugu, Binamu na wengineo, ni tamaduni isiyofaa. Tuwaambie Wachezaji wanaochipukia kuwa wanatakiwa kuwa imara na kufanya maamuzi ya fedha zao.”

Anadai yeye pia alikuwa mwathirika wa hali hiyo kuanzia alipoanza kufanikiwa kisoka, miaka mitano iliyopita aligeuka kuwa adui kwa ndugu baada ya kusitisha kutoa fedha

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here