Home KITAIFA HERSI ASHINDWA KUFAFANUA JAMBO HILI LA UBINGWA WA YANGA

HERSI ASHINDWA KUFAFANUA JAMBO HILI LA UBINGWA WA YANGA

0
Hersi

Rais wa Klabu ya Yanga, Eng. Hersi Said amepata kigugumizi na kushindwa kusema iwapo msimu huu watachukua ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC.

Akizungumza kufutaia matokeo mazuri waliyoyapata baada ya kuwafunga wapinzani wao, Simba Sc kwa bao 5-1.

“Mashabiki wana nafasi ya kufurahia na furaha zao zikaenda mbali zaidi wakasema tutachukua tena ubingwa msimu huu. Mimi kwangu ninaona kama ni dua njema na tunamuomba Mwenyezi Mungu tuchukue ubingwa kweli kwa sababu ndiyo malengo yetu.

“Lakini bado ni mapema sana, huu ni mchezo wetu wa tisa, hata moja ya tatu ya Ligi haijafika. Matokeo haya yanaweza kutupelekea tukawa kwenye nafasi nzuri lakini haiwezi kutupa ubingwa. Safari bado ni ndefu na msimu utakuwa mgumu sana.

“Ukitazama ratiba zilivyo mpaka sasa tumecheza mechi 9 na hakutakuwa na mechi tena Novemba baada ya Coasta Union. Mpaka katikati ya Desemba tutakuwa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, kisha siku chache za kucheza Ligi Desemba.

“Januari nzima tutakwenda Mapinduzi Cup kisha tutakwenda AFCON, kwa hiyo hakutakuwa na mechi za Ligi, tutarudi Februari.

“Ukitazama kuanzia Februari mpaka Juni ni miezi mine na kutakuwa na mechi 18 za Ligi, maana yake wiki zitakuwa 16 hivyo kuna wakati tutalazimika kucheza mechi zaidi ya moja ndani ya wiki moja,” amesema Eng. Hersi.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here