Home KITAIFA INJINIA HERSI ATOA AHADI NZITO

INJINIA HERSI ATOA AHADI NZITO

0
Hersi Said

RAIS wa Yanga, Injinia Hersi Said, amewataka mashabiki wa timu hiyo kujivunia timu yao, huku akitamka kuwa upo uwezekano mkubwa wa kupata ushindi wa mabao zaidi ya matano msimu huu watakapokutana tena na Simba.

Jeuri hiyo imekuja baada ya wikiendi iliyopita, Yanga kufanikiwa kuifunga Simba mabao 5-1 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Katika dabi hiyo, mabao ya Yanga yalifungwa na Kennedy Musonda, Stephene Aziz Ki, Pacome Zouzoua na Maxi Nzengeli aliyepachika mawili, huku la Simba likipachikwa na Kibu Denis.

Akizungumza na Spoti Xtra, Hersi alisema kama wakiendelea kupata ushirikiano mzuri kutoka kwa mashabiki wao, basi hakuna kitakachoshindikana kwao kupata idadi hiyo kutokana na mikakati waliyonayo uongozi.

Hersi alisema wao kama uongozi watatimiza majukumu yao ya kuiandaa timu yao, ikiwemo kambi nzuri, posho na mishahara watakayoitoa kwa wachezaji kwa wakati.

Aliongeza kuwa, anaamini kama uongozi ukitimiza mahitaji yao kwa wachezaji, basi vijana wao watahakikisha wanapambana na kupata matokeo mazuri ya ushindi mkubwa.

“Upo uwezekano mkubwa wa hizi tano tulizowafunga Simba katika Kariakoo Dabi zikajirudia zaidi ya hizo. Kikubwa uongozi tunataka ushirikiano mkubwa kutoka kwa mashabiki wetu ambao mara nyingi wamekuwa wakijitokeza uwanjani kuisapoti timu yao inapocheza.

“Sapoti hii iendelee ya mashabiki wetu, wakati wakiendelea kufurahia ushindi huo mkubwa wa mabao 5-1 tuliowafunga watani wetu wa jadi, Simba,” alisema Hersi.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here