Home KITAIFA JOB KUTOKA NDOTO MPAKA MAFANIKIO

JOB KUTOKA NDOTO MPAKA MAFANIKIO

0
job

Ilikuwa kama utani vile wengine waliona ndoto na wapo waliohisi haiwezekani lakini kijana kutoka Morogoro huko aliamini kuwa inawezekana kama tu ataamua ku focus na kilichomleta mjini kutoka kwenye mashamba ya miwa kule Mtibwa Sugar.

Ukiangalia kwenye kikosi cha Yanga SC hivi karibuni kumekuwa na msingi imara sana wa eneo la ulinzi, Kocha Nabi alianza kujenga huo ukuta Gamondi akaja kuendeleza alichokifanya Nabi ni kama tu Clouds ya marehemu Ruge bado inaendelea kufanya vizuri chini ya Joseph Kusaga.

Walimu wote wawili kwa nyakati tofauti waliwahi kukiri kuwa kama wanataka kucheza mpira wa kuanzisha mashambulizi kuanzia nyuma basi kwenye hiyo timu Dickson Job lazima aanze kwasababu ya uwezo wake mkubwa wa kutulia na mali mguuni na kuanzisha mashambulizi, mnaita footwork sio? Yes mtoto wa Morogoro anayo hiyo footwork.

Akili ya Yanga sc kwenye eneo la ulinzi ipo chini ya Dickson Job ukitaka kuamini maneno yangu subiri siku Yanga ikiwa inacheza halafu uwe na kazi moja ya kumuangalia Job akiwa uwanjani hapa ndo utaelewa kuwa huyu kijana ni muhimu pale jangwani zaidi ya gitaa kwa muimba kwaya.

Wengi walienda mbali na kuamua kumuita Big Brain Defender hii kwa lugha yetu pendwa ya Kiswahili maana yake ni beki mwenye akili kubwa mno uwanjani, ni mara chache kumuona Job akipata kadi uwanjani hii inaonesha ni kwa namna gani anacheza kwa nidhamu kubwa akiwa uwanjani.

Tuzo ya beki bora msimu uliopita hakuchukua kwa bahati mbaya kule Tanga ni kwasababu ya jitihada zake na kujituma kwake akiwa uwanjani Job ni moja kati ya wachezaji wenye muendelezo wa ubora, tangu aanze kuitwa timu ya taifa hajawahi kuachwa, na sasa ni nahodha msaidizi pale jangwani bado inakupa majibu kuwa ni moja kati ya vijana wanye nidhamu kubwa na kiwango bora kwasasa.

Anaweza kuonekana anafanya kitu cha kawaida kwasababu hajashuka terminal 3, wala passport yake haionyeshi katokea afrika magharibi huyu ni kijana kutoka mkoa wa karibu kabisa hapo Morogoro ila kazi yake uwanjani anawazidi hata baadhi ya wachezaji walioshuka terminal 3.

NB. Go East Go West ila kwasasa Dickson Job ni moja kati ya walinzi bora kwenye ligi yetu.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here