Home KITAIFA KIEMBA AFUNGUKA KILICHOWAPONZA SIMBA

KIEMBA AFUNGUKA KILICHOWAPONZA SIMBA

0
Kiemba simba

Mchambuzi wa soka Amri Kiemba, amesema kilichosababisha Simba washushiwe kipigo na Yanga ni baada ya Wekundu hao kuacha kuwaheshimu wapinzani wao.

“Pamoja na Yanga kuwa kwenye kiwango bora jana, lakini kuna nyakati ambazo Simba ilionekana kuwa bora na kutengeneza nafasi ambazo hawakuweza kuzitumia kufunga.

“Mambo yalianza kubadilika kwa Simba baada ya kuanza kuhisi wanaweza kupambana na Yanga uso kwa macho. Ukiangalia muda wote wa kipindi cha kwanza Mohamed Hussein alikuwa havuki mstari wa katikati kwenda upande wa Yanga.

“Kipindi cha kwanza Ngoma pia alikuwa anacheza karibu sana na walinzi wa nne wa Simba, washambuliaji wa Yanga ilikuwa ni ngumu kupokea mpira na kupata nafasi kati ya kiungo wa ulinzi wa Simba na mabeki.

“Muda ulivyokuwa unazidi kwenda Mohamed Hussein akajikuta anakwenda kushambulia kwenye eneo la Yanga, Ngoma na yeye akawa anasogea juu kidogo na hapo ndio zilipoanza kupatikana nafasi kwa wachezaji wa Yanga kukimbia nyuma ya mabeki wa Simba.”

Yanga wamekuwa hatari wanapopata nafasi ya kukimbia nyuma ya mabeki kuelekea goli la mpinzani, rejea magoli yote manne ya kipindi cha pili. Kipindi cha kwanza Simba waliziba nafasi hizo na hakukuonekana hatari nyingi za Yanga.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here