Home HABARI KIPIGO CHA MNYAMA GUMZO BUNGENI

KIPIGO CHA MNYAMA GUMZO BUNGENI

0
bungeni

Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson ameipongeza klabu ya Yanga kwa ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Simba.

Pongezi hizo amezitoa leo bungeni, jijini Dodoma katika Mkutano wa 13, Kikao cha sita cha Bunge.

“Tunawapongeza Yanga kwa mpira mzuri waliocheza jana,” amesema Dk. Tulia

Hata hivyo, pongezi hizi za Dk. Tulia zimechagizwa zaidi na ishara za wabunge kumpungia Spika mkono.

“Waheshimiwa wabunge nilikuwa natafakari hapa, kumbe napungiwa mkono kuonesha kwamba jana Yanga wamefunga magoli matano.” Amesema Dk. Tulia

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here