Home KITAIFA KOCHA MPYA SIMBA AANZA KAZI

KOCHA MPYA SIMBA AANZA KAZI

0
cadena simba

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa kwa sasa upo kwenye mikono salama ya kocha wa muda ambaye amechukua mikoba ya Roberto Oliveira.

Kocha Oliveira ambaye alikomba tuzo ya kocha bora ndani ya ligi Oktoba kutokana na mwendo wake bora alikutana na mkono wa asante Novemba 7 ikiwa ni baada ya kupoteza mchezo wa ligi dhidi ya Yanga.

Novemba 5 2023 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 1-5 Yanga kikiwa ni kipigo kikubwa kwa Simba kukipata kutoka kwa watani zao wa jadi.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema, “Kocha Daniel Cadena ambae amekabidhiwa jukumu la kuingoza timu yetu kwa kipindi hiki ni Kocha mwenye wasifu na uwezo mkubwa akimiliki leseni ya juu kabisa ya mpira wa miguu UEFA A LICENCE amezanza kazi.

“Kipindi hiki ambacho tunatafuta kocha mpya timu ipo kwenye mikono salama ndani ya kikosi cha Simba,”.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here