Home KITAIFA KOCHA WA MOROCCO “MNA UWANJA MZURI”

KOCHA WA MOROCCO “MNA UWANJA MZURI”

0
Kocha mkuu wa Morocco

Kocha mkuu wa Morocco, Walid Regragui amesema kwamba kitu pekee amekipenda tangu amekuja Tanzania kwaajili ya mchezo wao dhidi ya Taifa Stars ni uwanja mzuri wa Benjamin Mkapa ambapo ndipo kesho saa 4 usiku itakapopigwa mechi yao ya Kufuzu Kombe la Dunia 2026

“Katika maisha yangu ya Ukocha naweza sema kitu kinachonikwaza awali kabla ya mchezo ni Uwanja, nikishauona tu haufai huwa sina amani tena.. viwanja baadhi ya Afrika sio vizuri lakini kwa Tanzania naona hiki cha kwao wamejitahidi..”

“Nilikuja nikiwa siifahamu Tanzania kwasababu ndio mara ya kwanza nafika hapa ila naweza sema kwa muda mchache niliokaa tayari nimeona hii palivyo.. pana hali ya hewa nzuri na sijui ni hiki kipindi tulichokuja sisi au ndio panakuwaga hivi mwaka mzima.”

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here