Home KITAIFA KUNA MAISHA BAADA YA DABI

KUNA MAISHA BAADA YA DABI

0
kariakoo dabi

MAISHA lazima yaendelee bila kujali jambo gani gumu ama jepesi litakutokea kwa wakati huo. Kikubwa kwa sasa kuelekea Kariakoo Dabi wachezaji kutambua kwamba kuna maisha baada ya mchezo huo.

Muhimu kwa kila mmoja kutambua ana nafasi kubwa ya kufanya vizuri. Kutimiza majukumu yake uwanjani kwa kucheza bila hofu.

Haya yote yatawezekana ikiwa kila mmoja ataongeza umakini kwake na kwa mpinzani. Mpira sio vita wala sio sehemu ya kuonyeshana visasi vya nje ya uwanja.

Zile njia za mpira zitabaki palepale na atakayetumia makosa ya mpinzani ana nafasi ya kupata ushindi. Kuna wakati mechi zilipokuwa zikiisha wachezaji walikuwa wanaambulia maumivu.

Sio kufungwa pekee ndani ya uwanja bali kuumizwa na wachezaji wenzao baada ya mchezo. Muda mwingine wakatumia kwa ajili ya kupambania hali zao hili sio sawa.

Muhimu kwa wachezaji wa Simba na Yanga kutambua ukubwa walionao pamoja na timu wanazchezea. Maisha ya mchezaji yanahitaji kuendelea na mwendelezo wake unapatikana kutokana na kucheza mpira.

Ikiwa mchezaji utampa maumivu wakati huu mwenzako kisa dakika 90 za kusaka pointi tatu haitakuwa vema. Ile kasumba ya kuomba msamaha baada ya mchezo kwenye mitandao ya kijamii muda wake umeisha.

Ni muda wa kufanya yote ya kiuungwana kwa vitendo ndani ya uwanja kwenye mechi ambazo mnacheza ili kuongeza ushindani kwenye mechi zote za ligi.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here