Home KITAIFA KWA JKT QUEENS KANYAGA TWENDE

KWA JKT QUEENS KANYAGA TWENDE

0
JKT Queens

Wawakilishi wa Tanzania 🇹🇿 kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika kwa timu za soka za wanawake, JKT Queens ina dakika 90 za kuamua hatima ya kutinga nusu fainali itakapokabiliana na SC Casablanca ya Morocco ikiwa ni mechi ya tatu ya makundi.

Mchezo huo utapigwa Uwanja wa Amadou Gon Coulibaly, Ivory Coast kuanzia saa 2 usiku na sare au ushindi utaivushwa timu hiyo kutinga nusu fainali kutoka Kundi A kuungana na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Matokeo ya sare au kushinda yataivusha JKT na kuingia kwenye historia kama ilivyofanya Simba Queens iliyoshiriki msimu uliopita na kumaliza nafasi ya nne, ikiwa ni mara ya kwanza kama ilivyo kwa wawakilishi hao wa Tanzania ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake (WPL) na ile ya Afrika Mashariki na Kati.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here