Home KIMATAIFA MENDY KUIBURUZA CITY MAHAKAMANI

MENDY KUIBURUZA CITY MAHAKAMANI

0
Benjamin Mendy

Mchezaji wa zamani wa klabu ya Manchester City, Benjamin Mendy aipeleka timu yake hiyo ya zamani kwenye mahakama ya ajira kutokana na timu hiyo kumkata zaidi ya mamilioni ya pauni kutoka kwenye mishahara bila ruhusa yake.

Inaelezwa kuwa City iliacha kumlipa Mendy Septemba 2021 baada ya kufunguliwa mashtaka na kuwekwa kizuizini kutokana na kesi kadhaa za ubakaji na jaribio la ubakaji dhidi yake hivyo baada ya mashtaka hayo kufutwa ndipo Mendy ameenda kuwashtaki City juu ya mshahara wake na kesi inatarajiwa itasikilizwa mwaka wa 2024.

Mendy aliachana na City na kujiunga na klabu ya Lorient inayoshiriki Ligue 1 ya huko Ufaransa mwanzoni mwa msimu huu na hadi sasa ameshacheza mechi tatu kama mchezaji wa ziada

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here