Home KITAIFA NYONI ATUMA UJUMBE SIMBA

NYONI ATUMA UJUMBE SIMBA

0
Erasto Nyoni

KIRAKA ndani ya kikosi cha Namungo, Erasto Nyoni ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba.

Nyoni ameibuka ndani ya Namungo msimu wa 2023/24 baada ya kupewa Thank You ndani ya kikosi cha Simba.

Leo Novemba 9 2023 Simba inatarajiwa kumenyana na Namungo ikiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Ikumbukwe kwamba Simba imetka kupoteza mchezo wake uliopita kwa kushuhudia ubao ukisoma Simba 1-5 Yanga.

Nyoni amesema:”Tunatambua aina gani ya timu ambayo tunakutana nayo, tunawaheshimu ila tunahitaji pointi tatu muhimu.

“Tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu na mbinu za ufundi ambazo tumepewa na benchi la ufundi tutazitumia kupata matokeo chanya,” amesema.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here