Kocha Mkuu wa Simba Roberto olivieira amesema anafahamu ubora wa Yanga upo katika eneo la kiungo hivyo amejipanga kuhakikisha hawachomoki katika eneo hilo watakapovaana kesho.
Robertinho amesema maandalizi yanaendelea vizuri kuelekea mchezo wa kesho lakini tayari amefahamu ubora wao upo eneo gani hivo anakwenda kuwabana katika eneo hilo ili wasipatae nafasi ya kucheza kama walivyozoeleka.
Katika hatua nyingine kocha huyo amesema kabla ya mchezo watu wengi wanatoa maoni yao na kuwa wajuaji lakini mchezo ukimalika ukiwa umepoteza basi lawama zote zinaelekezwa kwa koha hivyo atahakikisha anashinda ili kijiweka katika mazingira salama zaidi.
Amemaliza kwa kuwatuliza mashabiki wa Simba akisema atachagua wachezaji sahihi kwa ajili ya mchezo huo utakaopigwa katika Uwanja wa Benjamini Mkapa.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE