Home KITAIFA ROBERTINHO AUKUBALI MZIKI WA YANGA, ASEMA HAYA

ROBERTINHO AUKUBALI MZIKI WA YANGA, ASEMA HAYA

0
Robertinho Simba

Kocha Mkuu wa Simba SC, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amewapongeza wapinzani wao wa jadi Yanga SC kwa kushinda dabi waliyoipiga jana Novemba 5, 2023 na kuibuka na ushindi wa 5-1.

Akizungumzia mchezo huo mara baada ya kumalizika kwa Simba kupoteza kwa kichapo hicho kizito, Robertinho amesema, wachezaji wake kipindi cha kwanza walicheza vizuri lakini kipindi cha pili walikuwa wanaacha nafasi kubwa kwa mpinzani.

“Walikaa nyuma sana na kutoa nafasi kwa mpinzani kufunga magoli mawili haraka lakini kimsingi niwaponmgeze wapinzani, wamecheza vizuri kipindi cha pili na kushinda dabi,” alisema Robertinho.

Yanga wamezidi kujikita kileleni kwenye msimamo wa Ligi Kuu kwa kufikisha alama 21 wakiwa wamecheza michezo nane huku Simba akishika nafasi ya tatu akibaki na alama zake 18 kwa michezo yake saba aliyocheza.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here