Baada ya kipigo cha kulipwa kisasi ambacho wamekipata Simba kutoka kwa mtani wao Yanga kwenye mchezo namba 111 wa ligi kuu bara mchezo wa Kariakoo Derby katika uwanja wa Mkapa, ambao umepigwa November 5, 2023.
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba ameandika haya kupitia ukurasa wake wa Instagram:
”Tumezidiwa na mpinzani wetu na hatimae tumeadhibiwa, hakuna unachoweza kusema zaidi kukiri udhaifu kwa upande wetu.Hili limepita japo linaumiza na haliwezi kufutika katika mioyo yetu lakini muhimu ni kuganga yajayo
Tusipoteze focus, mbele yetu tuna mechi nyingi za kupigania malengo yetu
Tumepoteza mechi moja bado tuna mechi nyingine mbele za kupigania malengo yetu.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE