Shabiki wa Simba SC, anayejiita ‘King Laudit Mavugo’ kutoka Mbinga Ruvuma kabla ya Derby ya Kariakoo ya Novemba 5, 2023, aliahidi kutoa Kilo moja ya mchele kwa kila shabiki wa Yanga kama timu yake ya Simba SC ingefungwa na Yanga SC.
Baada ya Simba SC kufungwa magoli 5 – 1 na Yanga SC, mashabiki zaidi ya (200) wa Yanga SC walikwenda dukani kwake wakihitaji bidhaa hiyo aliyoahidi.
Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Aziza Mangosongo ndiye aliyemuokoa ‘mwamba’ huyo na masaibu ya ahadi yake baada ya kuagiza Jeshi la Polisi kumsaidia.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE