Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameipongeza timu ya Yanga kwa ushindi dhidi ya Simba katika mchezo wa Ligi kuu ya Tanzania Bara uliopigwa leo Novemba 5 Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Kupitia kurasa zake rasmi za Mitandao ya Kijamii Rais Samia ameandika;
“Hongereni Yanga kwa ushindi dhidi ya Simba katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara. Upinzani wenu wa jadi wa zaidi ya miaka 85 sasa ni sehemu muhimu ya burudani yetu. Mnawaleta pamoja na kwa namna kipekee, mamilioni ya Watanzania ndani na nje ya nchi yetu”.
Katika mchezo huo Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 5-1.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE