Home HABARI ZA SIMBA LEO YAO BABA LAO KUELEKEA KARIAKOO DABI

YAO BABA LAO KUELEKEA KARIAKOO DABI

0
yao

MWAMBA Yao Attohoula ni baba lao kuelekea Kariakoo Dabi kwa upande wa kutengeneza pasi za mabao kwenye mechi za Ligi Kuu Bara.

Ni Novemba 5 watani hao wa jadi wanatarajiwa kumenyana kwenye msako wa pointi tatu, Uwanja wa Mkapa.

Katika nyota wenye pasi nyingi za mabao kwa watani hawa wa jadi, Yao ambaye ni beki kawakimbiza wote kibindoni akiwa katengeneza jumla ya pasi nne huku akifunga bao moja.

Pasi yake ya nne alitoa kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Azam FC uliochezwa Uwanja wa Azam Complex alimpa mshikaji wake Aziz Ki aliyepachika bao la tatu na kukamilisha hat trick yake ya kwanza kwenye ligi.

Kwa upande wa Simba ni Luis Miquissone (Konde Boy) licha ya mwendo wake wa kusuasua katoa pasi tatu za mabao kiungo huyo ndani ya kikosi cha Simba. Pasi yake ya tatu alimpa mshikaji wake Moses Phiri dakika ya 65 alipopachika bao la pili dhidi ya Ihefu wakakomba pointi tatu mazima.

Yao ni baba lao kwenye kutoa pasi kwa watani hawa wa jadi hivyo majibu yanatarajiwa kuonekana Novemba 5 Uwanja wa Mkapa kwenye Kariakoo Dabi watakapokutana kwenye msako wa pointi tatu.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here