KITAIFA

JEMBE LA BENCHIKHA LACHIMBA MKWARA MZITO

KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Muivory Coast, Aubin Kramo ametaja siku atakayorejea kuichezea timu hiyo, huku akiahidi kuifanyia makubwa.

Kiungo huyo yupo nje ya uwanja muda akiuguza majeraha ya goti ambayo alifanyiwa operesheni. Nyota huyo alifanyiwa operesheni hiyo nchini Afrika Kusini baada ya Madaktari kushauri.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Kramo alisema kuwa rasmi anatarajiwa kurejea uwanjani mapema Machi, mwaka huu baada ya kupona kamili.

Alisema kuwa baada ya kurejea uwanjani atahakikisha anafunga bao lake la kwanza katika Ligi Kuu Bara au Ligi ya Mabingwa Afrika kama shukrani kwa mashabiki kumvumilia.

“Nawapenda mashabiki wa Simba ambao wamekuwa wavumilivu na kunifariji kwa kipindi chote nilichokaa nje ya uwanja.

“Hivyo nimewaandalia zawadi kwao kwa kufunga bao baada ya kurejea mwezi Machi, mwaka huu baada ya kupona,” alisema Kramo.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button