KITAIFA

KARIA: MALENGO YA TAIFA STARS NI KUCHEZA HATUA YA MTOANO

Rais wa Shirikisho la soka nchini (TFF), Wallace Karia amesema kuwa endapo Taifa Stars wakipata alama 3 kwenye mchezo mmoja na michezo mingine wakipata alama nzuri basi wanaamini timu hiyo ya Taifa inaweza kucheza hatua ya mtoano ya AFCON

“Tutakapopata alama tatu tu, uwezekano ni kwamba tutavunja rekodi nyingine na kucheza hatua ya mtoano, ila mimi nina hakika kwa mataarisho yaliyokuwepo na morali iliyopo kwa vijana wetu tunao uwezo wa kupata zaidi ya alama tatu kwenye kundi letu.” amesema Karia

Huku tarehe 17 January kwenye mchezo wa kundi F alilopo Taifa Stars watashuka dimbani kutupa karata yao ya kwanza dhidi ya Morocco, mchezo utakao pigwa majira ya saa 2 usiku kwa saa za afrika mashariki, kwenye dimba la Stade de San Pedro.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button