KITAIFA

MOLOKO AZIDI KUTEMA NYONGO TANGU AACHWE YANGA

Aliyekua Kiungo Mshambuliaji ‘WINGA’ wa Young Africans, Jesus Moloko, amesema anaondoka Tanzania huku akiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindani uliopo katika Ligi Kuu Bara.

Rasmi Young Africans mwanzoni mwa juma hili ilitangaza kuachana na winga huyo kwa makubaliano ya pande zote, baada ya kudumu katika kikosi chao kwa muda wa miaka mitatu.

Moloko, amesema hataisahau Ligi Kuu Tanzania Bara kutokana na ushindani wake, lakini pia mapenzi ya mashabiki kwa klabu zao na wachezaji.

“Nimeishi vizuri sana hapa Tanzania, sitaisahau ligi ya hapa, imekuwa na ushindani, na kikubwa namna mashabiki wanavyopenda vilabu na wachezaji wao, hili ni jambo la kujivunia sana kwa watanzania,” amesema Moloko.

Ameongeza kuwa anarudi nchini kwao kuanza maisha mapya ya soka na kila kitu kitajulikana baada ya kufika huko, kwa sababu bado ana uwezo wa kucheza soka kwa kiwango cha juu.

“Nitaendelea na maisha ya soka, kwa sasa narudi Congo (DRC), kujipanga, na najua nitapata timu muda ukifika, bado nitaendelea kucheza soka,” Moloko ameongeza.

Winga huyo pia ameushukuru uongozi wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na wachezaji wenzake kwa ushirikiano waliompatia katika muda wote akiwa ndani ya timu hiyo.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button