KIMATAIFA

TAIFA STARS LEO DHIDI YA MOROCCO, WATAKE WASITAKE WAARABU WATAKAA TU!.

Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ leo inakabiliwa na kibarua kigumu ikicheza mechi ya kwanza katika fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) mwaka huu dhidi ya Morocco.

Ugumu wa mchezo huo unachangiwa na ubora wa Morocco ambayo ndio timu inayoongoza kwa viwango Afrika, hilo likichagizwa kwa kiasi kikubwa na mafanikio ambayo iliyapata katika fainali za Kombe la Dunia 2022, ambapo iliandika historia ya kuwa timu ya kwanza Afrika kufika nusu fainali.

Kulingana na maandalizi ya Taifa Stars na namna kikosi tulivyokiona katika mechi ya kirafiki na Misri tunaamini kilikuwa ni kipimo bora katika kujiandaa kwenye michezo mikubwa kama hii na kiwango kile wakikiboresha na kupunguza makosa basi leo inawezekana mwarabu akaangusha pointi. Kila la Kheri Taifa Stars.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button