KIMATAIFA

TAIFA STARS MWANZO SIO MBAYA KAZI IENDELEE

KIVUMBI cha mechi za Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON ambapo siku ya jana kundi F ambalo yupo Taifa stars imechezeka michezo huku tukishuhudia TaifaStars pekee katika kundi akikubali kupokea kichapo cha goli 3 kutoka kwa Morocco ila mchezo kati ya Zambia na DR Congo wakigawana pointi moja moja.

Mwanzo sio mbaya Taifa Stars mpaka dakika ya 70 ilikuwa nyuma kwa bao 1-0 dhidi ya Morocco ambapo bao lilipachikwa dakika ya 29 na Ghanem, Dakika hiyo ya 70 Novatus Dismas akatolewa kwa kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa mbili za njano, japo Novatus amesema kuwa hakumgusa mchezaji faulo ya pili iliyompa kadi ya njano.

Mabao mawili yalifungwa ndani ya dakika mbili ilikuwa dakika ya 76 na 78 katika mchezo wa Kombe la Mataifa Afrika (AFCON), Aziz Eddine na Youssef En-nesyn hawa walimtungua kipa wa Stars, Aishi Manula ambaye alikuwa langoni.

Nahodha Mbwana Samatta hakukomba dakika zote 90 za mchezo nafasi yake ilichukuliwa na Fei Toto, Kazi bado inaendelea ambapo ikiwa kundi F mchezo ujao ni dhidi ya Zambia iliyogawana pointi mojamoja na DR Congo mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Januari 21.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button