KITAIFATETESI ZA USAJILI

YANGA KUSHUSHA MSHAMBULIAJI HUYU FUNGA KAZI

MWAMBA huyu hapa mshambuliaji wa kazi ndani ya kikosi cha Yanga ikiwa ni ingizo jipya katika dirisha dogo.

Anaitwa Joseph Guede raia wa Ivory Coast ambapo kafunga dirisha la usajili kwa upande wa Yanga katika dirisha dogo.

Yeye ni mshambuliaji wa Kati anakuja kuongeza nguvu kwenye eneo la ushambuliaji ndani ya Yanga.

Wakati anaingia mwamba Hafiz Konkoni anatoka kwa kutolewa kwa mkopo ndani ya Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi.

Mbali na Konkoni pia mzawa Crispin Ngushi yeye atakuwa ndani ya Coastal Union inayotumia Uwanja wa Mkwakwani Tanga Kwa mechi za nyumbani.

Ipo wazi kuwa ndani ya Yanga washambuliaji hao wote wawili hawakuwa na nafasi kikosi cha kwanza hivyo wanakwenda kupata changamoto mpya katika timu zao mpya nyingine tena.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button