KITAIFA

YANGA NA KMC KUKIPIGA MOROGORO, JUMAMOSI HII

Mtanange wa Yanga na KMC unatarajiwa kupigwa Jumamosi ijayo, na utachezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro huku Simba pia ikihusishwa kuutumia uwanja huo kwenye mechi za nyumbani.

Mtendaji Mkuu wa KMC, Daniel Mwakasungula alithibitisha hilo kama wenyeji wa mchezo huo, ya kwamba wanakwenda kuchezea Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

“Mchezo wetu tunakwenda kuchezea Jamhuri, hivyo mashabiki wetu tunaomba wajiandae kwenda huko kuisapoti timu yetu,”amesema.

Huku habari za ndani za chombo cha kuaminiki kutoka katika klabu ya simba zikisema kuwa, “Baada ya kumaliza mechi za Kanda ya Ziwa, tutautumia Uwanja wa Jamhuri, Morogoro kuchezea mechi za nyumbani,” kilisema chanzo hicho.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button